Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano ya utawala ghasibu wa Israel amedai kwamba, serikali ya Rwanda imeieleza Tel Aviv kwamba, inafikiria kuhamishia ubalozi wake kutoka Tel Aviv na kuupeleka huko Beitul-Muqaddas.
Gazeti la Jerusalem Post limeripoti kwamba, Yoaz Hendel Waziri wa Mawasiliano wa Israel ambaye siku ya Ijumaa alikutana na Rais Paul Kagame mjini Kigali aliitaka rasmi nchi hiyo ya Kiafrika ihamishie ubalozi wake katika mji wa Beitul-Muqaddas.
Hata hivyo Rais Kagame amemjibu waziri huyo kwa kumwambia, kutokana na kuwa kuhamishia ubalozi wake huko Beitul-Muqaddas ni changamoto kubwa kwa Kigali, serikali yake inahitaji muda zaidi kabla ya kuchukua uamuzi wa suala hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu pia Malawi iliripotiwa ikitangaza kuwa, ina mpango wa kufungua ubalozi katika mji mtukufu wa Quds huko Palestina unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Disemba mwaka 2017, Rais Donald Trump wa Marekani alichukua uamuzi wa upande mmoja wa kuutambua mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, na kutangaza kuhamishia ubalozi wa Washington mjini Beitul-Muqaddas.
Licha ya propaganda kubwa ya mpango huo, hadi sasa ni nchi mbili tu za Guatemala na Paraguay ndizo ambazo zimefuata mkumbo huo wa Marekani huku Paraguay ikibadilisha uamuzi na kuurejesha tena ubalozi wake huko Tel Aviv ikiwa imepita miezi michache tu baada ya kuupeleka huko Baytul-Muqaddas.
342/